As-Saaffaat 37:157
الصافاتفَأْتُوا۟ بِكِتَـٰبِكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Basi leteni Kitabu chenu kama nyinyi ni wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli. [157]
[157] Basi leteni hoja zenu, ikiwa mnazo hoja za katika Kitabu cha mbinguni, kama nyinyi ni wakweli katika hayo myasemayo na mnayo yahukumia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Iwapo mna hoja ndani ya kitabu kitokacho kwa Allah Mtukufu, basi kileteni, mkiwa ni wa kweli katika hilo neno lenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net