As-Saaffaat 37:154
الصافاتمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ
Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?. [154]
[154] Ni nini lilio kusibuni hata mkakata hukumu bila ya ushahidi? Vipi mnahukumu hivyo na hali ni upotovu ulio wazi?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni uamuzi mbaya sana mnaoutoa, enyi watu, wa kuwa Allah Mtukufu Ana watoto wa kike na nyinyi mna watoto wa kiume, na hali nyinyi hamridhiki nafsi zenu kuwa na watoto wa kike.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net