As-Saaffaat 37:141
الصافاتفَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُدْحَضِينَ
Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walioshindwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa. [141]
[141] Alipo wahama watu wake bila ya amri ya Mola wake Mlezi, akaliendea jahazi ambalo lilio kwisha sheheni pomoni, akalipanda. Jahazi likapatikana na mambo ikawajibikia lazima mmoja katika abiria atoswe kupunguza shehena yake. Kura ikamuangukia Yunus, akashindwa kwa kura. Akatoswa baharini kwa mujibu wa ada yao zama zile.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mawimbi makubwa yakaizunguka jahazi hiyo kila upande. Na watu waliokuwa wamepanda jahazi wakapiga kura ili kupunguza shehena ili wasizame. Yûnus akawa ni miongoni mwa wale walioshindwa kwa kura.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net