Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 37 · Aya ya 110

As-Saaffaat 37:110

الصافات

كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. [110]

[110] Mfano wa malipo kama haya ya kuwakinga na balaa ndivyo tunavyo walipa walio wema katika kufuata amri za Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kama tulivyomlipa malipo mema Ibrãhîm kwa utiifu wake kwetu na kufuata kwake amri yetu, ndivyo tutakavyowalipa wenye kufanya wema miongoni mwa waja wetu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Saaffaat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net