Yaseen 36:9
يسوَجَعَلْنَا مِنۢ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَـٰهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ
Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao. Na tumewafunika macho yao, kwa hivyo hawaoni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni. [9]
[9] Na tumewafanya wale walio zuwiwa wasione Ishara na dalili ni kama walio fungwa baina ya kuta mbili, na macho yao yakagubikwa, wasione yaliyo mbele yao wala yaliyo nyuma yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumeweka mbele ya makafiri kizuizi na nyuma yao kizuizi. Basi yeye ni kama wale waliyofungiwa njia mbele yao na nyuma yao, hapo tukayapofusha macho yao kwa sababu ya ukanushaji wao na kiburi chao, hivyo basi wakawa hawaoni usawa wala hawaongoki. Na kila mwenye kuukabili ulinganizi wa Uislamu kwa kuupa mgongo na kuufanyia ushindani, basi yeye ni mstahili wa kupata mateso haya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net