Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 77

Yaseen 36:77

يس

أَوَلَمْ يَرَ ٱلْإِنسَـٰنُ أَنَّا خَلَقْنَـٰهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ

Maana

Kwani mwanadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndiyo amekuwa ndiye mgomvi wa dhahiri!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri! [77]

[77] Je! Binaadamu anakataa kuwepo Mwenyezi Mungu na uweza wake, na haoni yeye kwamba Sisi, baada ya kuwa hata hayupo, tulimuumba kutokana na tone la manii dhalili? Na sasa amekuwa mkali wa kutukhasimu kwa uwazi kabisa?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani haoni mwanadamu anayekanusha kufufuliwa vile umbo lake lilivyoanza, akapata kuchukua dalili ya kuwa atarudishwa uhai, kwamba sisi tumemuumba kwa tone la manii lililopitia miongo tofauti mpaka akawa mkubwa, na ghafla anageuka kuwa ni mwingi wa kubisha aliyejitolea wazi kwa kujadiliana?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net