Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 75

Yaseen 36:75

يس

لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ

Maana

Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio askari wao, watahudhurishwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakao hudhurishwa. [75]

[75] Hiyo miungu ya uwongo haiwezi kuwasaidia kwa lolote Mwenyezi Mungu akiwatakia madhara. Kwani miungu hiyo haiwezi kunafiisha wala kudhuru. Bali wao kwa hiyo miungu isiyo weza kitu, ni kama askari walio tayarishwa kwa ajili ya kuwakhudumia na wa kuwalinda na madhara.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waungu hao hawawezi kuwasaidia wenye kuwaabudu wala kujisaidia wao wenyewe. Na washirikina pamoja na waungu wao wote watahudhurishwa kwenye adhabu, wakiwa baadhi yao wanajitenga na wengine.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net