Yaseen 36:73
يسوَلَهُمْ فِيهَا مَنَـٰفِعُ وَمَشَارِبُ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ
Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru? [73]
[73] Na wanapata kwa hao vitu vya kuwapa manufaa, kama sufi, na manyoya, na nywele, na ngozi, na mafupa, na vinywaji kutokana na maziwa yao. Je! Wanasahau neema hizi hata wamekuwa hawamshukuru aliye waneemesha?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na katika hao wanyama, wana manufaa mengine ya kunufaika nayo, kama vile kunufaika kwa sufi zao, mabele yao na nywele zao kwa matumizi ya nyumbani, mavazi na mengineyo, na wanakunywa maziwa yao. Basi hawamshukuru Allah Mtukufu, Ambaye Amewapa neema hizi, na kumtakasia ibada?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net