Yaseen 36:60
يسأَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا۟ ٱلشَّيْطَـٰنَ ۖ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ
Je, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwa msimuabudu Shet'ani? Hakika yeye ni adui dhaahiri kwenu. [60]
[60] Enyi wanaadamu! Sikukuusieni kuwa msimfuate Shetani kwa ut'iifu kama kwamba ni mungu wa kuabudiwa. Hakika yeye ni adui yenu, aliye dhihirisha uadui wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Atawaambia kwa kuwalaumu na kuwakumbusha, Kwani sikuwausia, kupitia ndimi za Mitume wetu kwamba msiabudu Shetani wala msimtii? Hakika yeye ni adui ambaye uadui wake umejitokeza wazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net