Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 51

Yaseen 36:51

يس

وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ ٱلْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ

Maana

Na litapulizwa baragumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi. [51]

[51] Na barugumu litapulizwa kwa mpulizo wa kufufua watu. Mara watu watatoka makaburini mwao wakikimbilia kwenda kukutana na Mwenyezi Mungu. Na hilo barugumu, na kupulizwa kwake, ni katika anayo yajua Mwenyezi Mungu Yeye peke yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kutapulizwa baragumu mpulizo wa pili, hapo roho zao zirudishwe kwenye miili yao, wakitahamaki wanatoka makaburini mwao wakielekea kwa Mola wao kwa haraka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net