Yaseen 36:49
يسمَا يَنظُرُونَ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ
Hawangojei isipokuwa ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wamo kuzozana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukua nao wamo kuzozana. [49]
[49] Hawangojei ila sauti moja tu, iwamalize kwa ghafla, nao wakizozana katika mambo ya kidunia, wameghafilika na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawangojei hawa washirikina wanaolifanyia haraka agizo la Allah Mtukufu kwao, isipokuwa mpulizo wa fazaa wakati Kiyama kitakaposimama, kitawachukua ghafla, na hali wao wanagombana katika mambo ya maisha yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net