Yaseen 36:47
يسوَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنفِقُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنُطْعِمُ مَن لَّوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ أَطْعَمَهُۥٓ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ
Na wanapoambiwa: "Toeni katika aliyokupeni Mwenyezi Mungu", wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Je, tuwalishe wale ambao Mwenyezi Mungu angependa angeliwalisha mwenyewe? Nyinyi hammo isipokuwa katika upotovu ulio dhahiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo ambiwa: Toeni katika aliyo kupeni Mwenyezi Mungu, walio kufuru huwaambia walio amini: Je! Tuwalishe ambao Mwenyezi Mungu angependa angeli walisha mwenyewe? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhaahiri. [47]
[47] Na wakiambiwa: Wapeni mafakiri kutokana na hicho alicho kuruzukuni Mwenyezi Mungu, makafiri huwaambia Waumini: Je! Tuwalishe watu ambao Mwenyezi Mungu Mwenyewe angeli taka angeli walisha? Hivyo inakuwa tunamfanyia inda Mwenyezi Mungu kwenda kinyume na mapenzi yake! Nyinyi mnao taka tutoe, si chochote ila mmo katika upofu ulio wazi, hamuioni Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na waambiwapo makafiri, «Toeni ile riziki ambayo Allah Mtukufu Amewaneemesha nayo,» wanasema kuwaambia Waumini, wakijenga hoja, «Je, tumpe chakula yule ambaye lau Allah Mtukufu angetaka angempa chakula? Hamkuwa nyinyi, Waumini, isipokuwa mko mbali waziwazi na haki, kwa kutuamrisha sisi hilo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net