Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 45

Yaseen 36:45

يس

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّقُوا۟ مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

Maana

Na wanapoambiwa: Jilindeni kutokana na yaliyoko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa...

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa [45]

[45] Na wanapo ambiwa: Yaogopeni mfano wa yaliyo wapata mataifa yaliyo kwisha pita kwa kukadhibisha kwao, na iogopeni adhabu ya Akhera ambayo itakupateni kwa kushikilia kwenu ukafiri, kwa kutaraji kuwa asaa Mola wenu Mlezi akakurehemuni mkimcha Yeye, wao hupuuza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na washirikina wanapoambiwa, «Jihadharini na jambo la Akhera na vitisho vyake, hali za dunia na mateso yake, kwa kutarajia rehema za Allah Mtukufu kwenu,» wanapuuza na hawalikubali hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net