Yaseen 36:33
يسوَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلْأَرْضُ ٱلْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَـٰهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ
Na Ishara hiyo kwao ni ardhi iliyokufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanakula katika hizo!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazila! [33]
[33] Na dalili kwao ya uweza wetu wa kufufua ni kuangalia vipi ardhi yenye ukame tunavyo ihuisha kwa maji, na kutoa ndani yake nafaka wanazo zila.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ili kuwaonyesha hawa washirikina ushahidi wa uwezo wa Allah Mtukufu wa kufufua na kukusanya: ni hii ardhi iliyokufa isiyo na mimea, tumeihuisha kwa kuteremsha maji, na tukatoa humo aina mbalimbali za mimea ambayo watu na wanyama wanakula. Na Mwenye kuhuisha ardhi kwa mimea Ndiye Atakayehuisha viumbe baada ya kufa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net