Yaseen 36:30
يسيَـٰحَسْرَةً عَلَى ٱلْعِبَادِ ۚ مَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli. [30]
[30] Ee khasara yao, inayo faa kusikitikiwa! Hatuwapelekei waja wangu Mtume ila wao huwa wakimfanyia maskhara.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni hasara iliyoje na majuto yalioje ya waja Siku ya Kiyama watakapoiona adhabu! Hawajiwi na mtume yoyote kutoka kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, isipokuwa huwa wakimfanyia shere na maskhara.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net