Yaseen 36:28
يسوَمَآ أَنزَلْنَا عَلَىٰ قَوْمِهِۦ مِنۢ بَعْدِهِۦ مِن جُندٍ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ
Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha. [28]
[28] Na Sisi hatukawaangamiza kwa kuwapelekea maaskari kutoka mbinguni. Wala huo sio mtindo wetu kupeleka majeshi tunapo yahiliki mataifa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na jambo hilo halikuhitajia kuteremsha askari kutoka mbinguni ili kuwaadhibu wao baada ya wao kumuua yule mwanamume anayewapa ushauri mwema na kuwakanusha wajumbe wao, kwani wao ni wanyonge na watwevu zaidi kuliko kuwa ni wenye kufanyiwa hilo, na hatukuwa ni wenye kuwateremsha Malaika tukitaka kuwaangamiza, bali tunawateremshia adhabu ya kuwavunjavunja.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net