Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 26

Yaseen 36:26

يس

قِيلَ ٱدْخُلِ ٱلْجَنَّةَ ۖ قَالَ يَـٰلَيْتَ قَوْمِى يَعْلَمُونَ

Maana

Akaambiwa: "Ingia Peponi!" Akasema: "Laiti kuwa watu wangu wangelijua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua [26]

[26] Kuwa ni malipo ya Imani yake na wito wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ataambiwa: Ingia Peponi! Naye, hali yuko katika kivuli cha neema na hishima, atasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua alivyo nighufiria Mola wangu Mlezi na kunipa hishima, nao wakaamini kama nilivyo amini mimi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Aliambiwa baada ya kufa kwake, «Ingia Peponi,» kwa njia ya kutukuzwa, akasema: Natamani watu wangu wangejua.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net