Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 23

Yaseen 36:23

يس

ءَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً إِن يُرِدْنِ ٱلرَّحْمَـٰنُ بِضُرٍّ لَّا تُغْنِ عَنِّى شَفَـٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا يُنقِذُونِ

Maana

Je, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani (Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa. [23]

[23] Je! Niishike kwa kuiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, miungu mingine isiyo nifaa kitu kuniombea kwao, pindi Mwenyezi Mungu akinitakia madhara? Wala hawataniokoa nayo yakinishukia hayo madhara.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, niwaabudu waungu wengine wasiomiliki jambo lolote badala ya Allah Mtukufu? Iwapo Mwingi wa rehema Amenitakia mabaya, basi waungu hawamiliki kulikinga hilo wala kulizuia, wala hawawezi kuniokoa mimi na haya niliyonayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net