Yaseen 36:21
يسٱتَّبِعُوا۟ مَن لَّا يَسْـَٔلُكُمْ أَجْرًا وَهُم مُّهْتَدُونَ
Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka. [21]
[21] Wafuateni watu wasio taka kwenu ujira wowote kwa kukunasihini na kukuongozeni, na hali wao wenyewe wameongoka, na nyinyi mtapata manufaa kwa kufuata njia ya kheri na mafanikio!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wafuateni wale wasiotaka mali kutoka kwenu kwa kufikisha Ujumbe, na hali wao wako kwenye uongofu katika kile wanachowaitia cha kumuabudu Allah Mtukufu Peke Yake. Katika aya hii kuna kueleza ubora wa mwenye kukimbilia kuamrisha mema na kukataza maovu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net