Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 36 · Aya ya 19

Yaseen 36:19

يس

قَالُوا۟ طَـٰٓئِرُكُم مَّعَكُمْ ۚ أَئِن ذُكِّرْتُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ

Maana

Wakasema: "Mkosi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu waliopindukia mipaka."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukia mipaka. [19]

[19] Wale Wajumbe wakasema: Ukorofi mnao nyinyi wenyewe, kwa hizo kufuru zenu. Badala ya kuwaidhika kwa mambo yenye kheri kwenu wenyewe, mnatutuhumu sisi kuwa ni wakorofi, na mnatutishia kutupa adhabu chungu? Lakini nyinyi ni watu mlio pindukia mipaka ya Haki na Uadilifu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wajumbe wakasema, Kisirani chenu na matendo yenu ya ushirikina na ya shari yako na nyinyi na yanarudishwa kwenu nyinyi. Je, nyinyi mkiwaidhiwa kwa jambo ambalo lina kheri kwenu mnajihisi mmeingiliwa na kisrani na mnatutisha kuwa mtatupiga mawe na kutuadhibu? Bali nyinyi ni watu ambao desturi yenu ni kupita kiasi katika uasi na ukanushaji.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yaseen

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net