Faatir 35:25
فاطروَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ جَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ وَبِٱلزُّبُرِ وَبِٱلْكِتَـٰبِ ٱلْمُنِيرِ
Na wakikukadhibisha, basi walikwisha kanusha wale waliokuwa kabla yao. Mitume wao waliwajia kwa ushahidi wa waziwazi na kwa maandiko na Kitabu chenye nuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakikukanusha basi walikwisha wakanusha walio kuwa kabla yao. Mitume wao waliwajia kwa dalili wazi wazi na kwa maandiko na Kitabu chenye nuru. [25]
[25] Na ikiwa kaumu yako wanakukadhibisha wewe basi walio kuwa kabla yao waliwakadhibisha Mitume wao vile vile. Na wao waliwaletea miujiza iliyo wazi, na Maandiko ya Mola Mlezi na Kitabu chenye nuru kwa ajili ya kuwaongoza Njia ya kuokoka duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanapokukanusha washirikina hawa, basi wale waliopita kabla yao waliwakanusha Mitume wao ambao waliwajia na miujiza iliyo wazi yenye kutolea ushahidi unabii wao, na waliwajia na Vitabu, ambavyo ndani yake zimekusanywa hukumu nyingi, na (waliwajia na) Kitabu chenye kutoa mwangaza, chenye kubainisha njia ya kheri na shari.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net