Faatir 35:18
فاطروَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَىٰ حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَىْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰٓ ۗ إِنَّمَا تُنذِرُ ٱلَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِٱلْغَيْبِ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ ۚ وَمَن تَزَكَّىٰ فَإِنَّمَا يَتَزَكَّىٰ لِنَفْسِهِۦ ۚ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلْمَصِيرُ
Na mbebaji hatabeba mzigo wa mwengine. Na aliyetopewa na mzigo wake akiomba uchukuliwe, hautachukuliwa hata kidogo, hata kama ni jamaa yake. Hakika wewe unawaonya wale wanaomcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Swala. Na mwenye kujitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Na aliye topewa na mzigo wake akiomba uchukuliwe hautachukuliwa hata kidogo, na angamwomba jamaa yake. Hakika wewe unawaonya wale wanao mcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Swala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu. [18]
[18] Wala nafsi yenye dhambi haitobeba dhambi za mwenginewe. Na mtu aliye kuwa taabani kwa mzigo wake wa madhambi, akimwomba mwenginewe amchukulie, huyo mwengine hatomchukulia hata kidogo, hata angeli kuwa ni jamaa yake. Haya ni kwa kuwa kila mtu kashughulika na yake. Na ewe Nabii! Usihuzunike kwa inadi ya watu wako. Kwani hakika maonyo yako yanawafaa wale ambao wanamkhofu Mola wao Mlezi peke yao katika siri, na wakashika Swala kwa mujibu inavyo faa. Na mwenye kujisafisha na uchafu wa madhambi, basi anajisafisha kwa faida ya nafsi yake. Na marejeo yote mwishoni ni kwa Mwenyezi Mungu, na Yeye atamtendea kila mtu kwa anavyo stahiki. Rejea maoni ya ki-ilimu juu ya Aya 7 Surat Azzumar: Na mbebaji habebi mzigo wa mwengine.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kiumbe yoyote Aliyefanya dhambi hatabeba dhambi za mtu mwingine. Na mtu yoyote aliyelemewa na dhambi, akiomba mwenye kumbebea dhambi zake, hatapata mwenye kumbebea chochote, hata kama yule aliyemuomba ana ujamaa wa karibu na yeye, kama baba au ndugu na mfano wao. Hakika ni kwamba wewe, ewe Mtume, unawaonya wale wanaoogopa adhabu ya Mola wao pamoja na kuwa wao hawaioni na wakatekeleza Swala inavyotakikana itekelezwe. Na mwenye kujisafisha na ushirikina na maasia mengine, basi yeye anajisafisha nafsi yake. Na kwa Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ndio marejeo ya viumbe wote na mwisho wao, hapo Amlipe kila mmoja kile anachostahiki
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net