Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 54

Saba 34:54

سبإ

وَحِيلَ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ مَا يَشْتَهُونَ كَمَا فُعِلَ بِأَشْيَاعِهِم مِّن قَبْلُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ فِى شَكٍّ مُّرِيبٍۭ

Maana

Na watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani, kama walivyofanyiwa wenzao zamani. Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayo yatamani, kama walivyo fanyiwa wenzao zamani. Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi. [54]

[54] Patawekewa kizuizi baina yao na hayo wanayo yatamani ya Imani ya kuwafaa, kama walivyo fanyiwa wenzao wa kabla yao walipo amini baada ya kwisha wakati wake. Kwa sababu wote hao wote walikuwa katika kuifanyia Haki shaka inayo pelekea kutuhumiwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kutawekwa kizuizi baina ya wakanushaji na kile wanachokitamani cha toba na kurudi ulimwenguni wapate kuamini, kama vile Allah Mtukufu Alivyowafanya wale wanaofanana na wao miongoni mwa wakanushaji wa watu wa mataifa yaliyopita. Kwa kweli wao walikuwa duniani wako kwenye shaka yenye kutia wasiwasi na babaiko kuhusu jambo la Mitume, kufufuliwa na kuhesabiwa, na kwa hivyo hawakuamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net