Saba 34:3
سبإوَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَا تَأْتِينَا ٱلسَّاعَةُ ۖ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّى لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَـٰلِمِ ٱلْغَيْبِ ۖ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَلَآ أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكْبَرُ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ مُّبِينٍ
Na walisema wale waliokufuru: "Haitatufikia Saa ya Kiyama." Sema: Kwani, hapana shaka itakufikieni, ninaapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi, isipokuwa vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walisema walio kufuru: Haitatufikia Saa (ya Kiyama). Sema: Kwani? Hapana shaka itakufikieni, naapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinacho fichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi; ila vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha. [3]
[3] Na wenye kukufuru wakasema: Haitujii Saa iliyo ahidiwa kuwa ni ya kufufuliwa na kukusanywa watu. Waambie ewe Mtume! Hapana shaka itakujieni, nami naapa kwa Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya siri, ambaye hapana chenye kughibu na ujuzi wake hata ingawa kiasi ya chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi. Wala kilicho kidogo kuliko chembe, wala kikubwa kuliko hivyo hakikosi kuandikwa katika Kitabu kilicho timia, chenye kubainisha kila kitu. Dharra , tuliyo ifasiri "Chembe", na kisayansi ni Atom kwa hakika katika lugha ya Kiarabu ni kitu kidogo sana, kama sisimizi mdogo, au chembe ya vumbi. Na uzito wa Dharra maana yake ni uzani wake. Na Aya inaonyesha kuwa kipo kilicho kuwa ni kidogo kuliko Dharra. Na yafaa kutaja hapa kuwa sayansi za sasa zimethibitisha kuwa Dharra, yaani Atom, imegawika katika sehemu ndogo zaidi nazo ni Nucleus na Electrons. Na haya haya hayakuthibitika ila katika karne ya ishirini ya kuzaliwa Nabii Isa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na makafiri wenye kukanusha kufufuliwa walisema. «Kiyama hakitatujia.» Sema, ewe Mtume, uwaambie! Ninaapa kwa Mola wangu, kitawajia! Lakini hakuna yoyote anayejua wakati wa kuja kwake isipokuwa Allah Mtukufu, Mjuzi wa visivyoonekana, Ambaye haufichiki Kwake uzito wa kadiri ya mdudu chungu uliyo mbinguni au ardhini, hata mdogo zaidi kuliko huo na hata mkubwa, isipokuwa uko kwenye Kitabu kilichotunzwa, nacho ni Ubao Uliohifadhiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net