Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 4

Al-Ahzaab 33:4

الأحزاب

مَّا جَعَلَ ٱللَّهُ لِرَجُلٍ مِّن قَلْبَيْنِ فِى جَوْفِهِۦ ۚ وَمَا جَعَلَ أَزْوَٰجَكُمُ ٱلَّـٰٓـِٔى تُظَـٰهِرُونَ مِنْهُنَّ أُمَّهَـٰتِكُمْ ۚ وَمَا جَعَلَ أَدْعِيَآءَكُمْ أَبْنَآءَكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ قَوْلُكُم بِأَفْوَٰهِكُمْ ۖ وَٱللَّهُ يَقُولُ ٱلْحَقَّ وَهُوَ يَهْدِى ٱلسَّبِيلَ

Maana

Mwenyezi Mungu hakumwekea mwanamume yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayesema kweli, naye ndiye anayeongoa Njia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye sema kweli, naye ndiye anaye ongoa Njia. [4]

[4] Mwenyezi Mungu hakumjaalia mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake; wala hakumfanya mke wa yeyote katika nyinyi kuwa ni mama yake, pale anapo sema ati: Wewe kwangu mimi kama mgongo wa mama yangu! Wala hakuwafanya watoto mnao wapanga kuwa ni wenenu, kuwa hakika ni wana wenu kwa nasaba. Hayo ya kuwafanya watoto wa kupanga kuwa ni wenenu, ni kauli inayo toka kwenye vinywa vyenu, wala hayana ukweli. Hapana hukumu yoyote inayo tokana na hayo. Na Mwenyezi Mungu anasema jambo lilio thibiti la hakika. Na anakuongozeni mlifikie. Na Yeye peke yake Subhanahu ndiye anaye ongoa watu kwenye Njia iliyo sawa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu hakumfanya yoyote miongoni mwa wanadamu awe na nyoyo mbili kifuani mwake, na hakuwafanya wake wenu mnaojiharamisha nao kwa njia ya ẓihār kama vile uharamu wa mama zenu. (Ẓihār ni mwanamume kumwambia mkewe, ‘Wewe ni haramu kwangu kama vile mgongo wa mamangu.) Na hii ilikuwa ni talaka katika kipindi cha ujinga (kabla ya kuja Uislamu) na Allah Mtukufu Akabainisha kwamba mke hawi mama kwa namna yoyote. Na Allah Mtukufu Hakuwafanya watoto wa kupachika kuwa ni watoto katika sheria. Bali ufananishaji na mgongo na upachikaji watoto, viwili hivyo havina uhakika katika uharamishaji wa milele, kwani mke aliyefananishwa na mgongo wa mama hawi ni kama mama katika uharamu, na nasaba haithibiti kwa kujipachika watoto kwa mtu kusema kuhusu mtoto wa kulea, «Huyu ni mwanangu». Kwani haya ni maneno ya mdomo yasiyo na ukweli na hayazingatiwi. Na Allah Mtukufu Anasema haki na Anawabainishia waja Wake njia Yake na Anawaongoza njia ya uongofu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net