Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 32 · Aya ya 18

As-Sajda 32:18

السجدة

أَفَمَن كَانَ مُؤْمِنًا كَمَن كَانَ فَاسِقًا ۚ لَّا يَسْتَوُۥنَ

Maana

Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa. [18]

[18] Kwani watu watakuwa sawa katika malipo yao, na hali wamekhitalifiana katika vitendo vyao? Je! Aliye kuwa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu ni kama mwenye kumkataa na akamuasi? Hasha! Hawawi sawa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, Yule Aliyekuwa mtiifu kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake, mwenye kuamini agizo lake la kuwalipa mema wema wenye kufanya mema na kuwalipa ubaya wenye kufanya mabaya, ni kama yule aliyemkanusha Allah Mtukufu na Mitume Yake na akaikanusha Siku ya Kiyama? Hawalingani mbele ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

As-Sajda

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net