Luqman 31:33
لقمانيَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمْ وَٱخْشَوْا۟ يَوْمًا لَّا يَجْزِى وَالِدٌ عَن وَلَدِهِۦ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِۦ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِٱللَّهِ ٱلْغَرُورُ
Enyi watu, mcheni Mola wenu Mlezi, na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi yasiwadanganyeni maisha ya dunia, wala asiwadanganyeni na Mwenyezi Mungu yule mdanganyifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi, na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala asikudanganyeni na Mwenyezi Mungu mdanganyifu. [33]
[33] Enyi watu! Fanyeni aliyo kuamrisheni Mola wenu Mlezi, na wacheni aliyo kukatazeni. Na tahadharini na adhabu yake ya Siku ya Kiyama, Siku ambayo kwamba mzazi hatamfaa mwanawe kwa lolote, wala mwana hatamfaa mzazi wake kwa lolote. Hakika Siku hii ndiyo aliyo iahidi Mwenyezi Mungu. Na ahadi yake ni ya kweli, hayendi kinyume. Basi yasikupumbazeni mapambo ya dunia na uzuri wake, mkaacha kujitayarisha kwa ajili ya Siku hiyo. Wala msikhadaike na uchochezi wa Shetani, ukakuachisheni kumuelekea Mwenyezi Mungu na kumt'ii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi watu! Mcheni Mola wenu na mtiini kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, na jihadharini na Siku ya Kiyama ambayo mzazi hatamfaa kitu mwanae, wala mwana hatamfaa kitu baba yake. Hakika ahadi ya Allah Mtukufu ni kweli haina shaka, basi msihadaike na uhai wa duniani na pambo lake, ukawafanya msahau uhai mwingine. Na asiwahadae nyinyi yoyote mwenye kuhadaa miongoni mwa mashetani wa kibinadamu na wa kijini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net