Luqman 31:26
لقمانلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ٱلْحَمِيدُ
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mkwasi, Mwenye kusifiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mkwasi, Mwenye kusifiwa. [26]
[26] Viliomo katika mbingu na ardhi ni vya Mwenyezi Mungu, kwa kuviumba, na kuvikadiria, na kuvipanga. Basi vipi wao wanaacha kumuabudu Yeye? Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika si mhitaji wa viumbe vyake wala ibada yao. Yeye ni Msifiwa kwa dhati yake. Ni mwenye kustahiki kusifiwa na waja wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni vya Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, vyote vilivyoko mbinguni na ardhini kwa kuvimiliki, kuvifanya vifuate amri, kuvipatisha na kuvipangia mambo yake, hivyo basi hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Hakika Allah Mtukufu Ndiye Mkwasi Anayejitosheleza mwenyewe Asiyehitaji viumbe Vyake. Ni Zake Yeye shukrani na sifa njema kwa kila namna.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net