Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 31 · Aya ya 19

Luqman 31:19

لقمان

وَٱقْصِدْ فِى مَشْيِكَ وَٱغْضُضْ مِن صَوْتِكَ ۚ إِنَّ أَنكَرَ ٱلْأَصْوَٰتِ لَصَوْتُ ٱلْحَمِيرِ

Maana

Na kuwa wa hali ya katikati katika kutembea kwako, na teremsha chini sauti yako. Hakika katika sauti mbaya kuliko zote ni sauti ya punda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda. [19]

[19] Na nenda mwendo wa wastani, si mbio mbio mno wala taratibu mno. Na teremsha sauti yako. Kwani hapana sauti mbaya kama sauti ya punda. Inaanzia kwa mngurumo unao ghasi, na inaishia kwa ukenje unao kera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na unyenyekee katika kwenda kwako na uishukishe chini sauti yako usiipandishe juu, kwani sauti mbaya zaidi na inayochukiza zaidi ni sauti ya punda wanaojulikana kwa upumbavu wao na sauti zao za juu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Luqman

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net