Luqman 31:12
لقمانوَلَقَدْ ءَاتَيْنَا لُقْمَـٰنَ ٱلْحِكْمَةَ أَنِ ٱشْكُرْ لِلَّهِ ۚ وَمَن يَشْكُرْ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ
Na tulimpa Luqman hekima, tukamwambia; "Mshukuru Mwenyezi Mungu." Na mwenye kushukuru, basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliyekufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tulimpa Luqman hikima, tukamwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu. Na mwenye kushukuru basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliye kufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa. [12]
[12] Na hakika tulimpa Luqman hikima, na ilimu, na kauli ya kusibu. Tulimwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema aliyo kupa. Na mwenye kushukuru basi hakika huyo anaitafutia kheri nafsi yake. Na mwenye kuzikufuru neema, akazikataa, na asishukuru kwa ajili yake, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuihitaji shukra yake, na Yeye Mwenyezi Mungu ni Mwenye kustahiki sifa zote njema, na ingawa pasiwepo hata mmoja wa kumsifu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika tulimpa mja mwema miongoni mwa waja wetu, naye ni Luqmān, busara, nayo ni ufahamu wa Dini, akili na usawa wa maneno, na tulimwambia, Zishukuru neema za Allah Mtukufu juu yako. Na Mwenye kumshukuru Mola wake, faida yake itamrudia mwenyewe, na Mwenye kukanusha neema Zake, basi Allah Mtukufu ni Tajiri, Hahitaji kushukuriwa, ni Zake Yeye shukrani na sifa njema kwa kila hali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net