Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 31 · Aya ya 10

Luqman 31:10

لقمان

خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ وَأَلْقَىٰ فِى ٱلْأَرْضِ رَوَٰسِىَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَآبَّةٍ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ

Maana

Ameziumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona, na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isiwayumbishe, na ametawanya humo kila namna ya wanyama, na tumeteremsha maji kutoka mbinguni, na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ameziumba mbingu bila ya nguzo mnazo ziona; na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isikuyumbisheni; na ametawanya humo kila namna ya wanyama; na tumeteremsha maji kutoka mbinguni, na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna. [10]

[10] Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu zisio na nguzo za nyinyi kuziona. Na juu ya ardhi ameweka milima iliyo simama imara, ili ardhi isikutingisheni. Na humo katika ardhi ametawanya kila namna ya wanyama wanao tambaa na kwenda. Na tumeteremsha maji kutoka mbinguni, na tukaotesha mimea ya kila namna nzuri yenye manufaa katika ardhi. Rejea uangalie maelezo ya kisayansi juu ya Aya 2, Sura ya Ar-Raa'd.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ameumba mbingu, Akaziinua bila ya nguzo kama mnavyoziona. Na Ameweka ndani ya ardhi majabali yaliyojikita, ili zisipate kutikisika na kutetemeka yakaharibika maisha yenu. Na Ameeneza kwenye ardhi aina mbalimbali za wanyama. Na tumeteremsha kutoka mawinguni mvua, tukaotesha kwayo kwenye ardhi kila aina ya mimea mizuri yenye nafuu yenye mandhari nzuri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Luqman

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net