Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 31 · Aya ya 1

Luqman 31:1

لقمان

الٓمٓ

Maana

Alif Laam Miim.[1]

[1] Herufi hizi "Alif Laam Miim" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alif Lam Mim (A.L.M.) . [1]

[1] Harufi hizi zimeanzia baadhi ya Sura kuashiria kuwa Qur'ani ni muujiza ulio tungwa na harufi kama harufi wanazo zitumia Waarabu katika maneno yao. Na juu ya hayo wao wameshindwa kuleta mfano wake. Na pia ni kwa ajili ya kuzindua watu wasikilize na watege sikio. Na washirikina walikuwa wamewafikiana kuwa wawe wanaropokwa maneno ya upuuzi tu ikisomwa Qur'ani wala wasiisikilize.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Alif, Lām, Mīm» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al- Baqarah.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Luqman

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net