Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 55

Ar-Room 30:55

الروم

وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يُقْسِمُ ٱلْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا۟ غَيْرَ سَاعَةٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَانُوا۟ يُؤْفَكُونَ

Maana

Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, wahalifu wataapa kwamba hawakukaa duniani isipokuwa saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakipotoshwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na siku itapo simama Saa wakosefu wataapa kwamba hawakukaa duniani ila saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyo kuwa wakipotozwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na siku kitakapokuja Kiyama na Atakapo Allah Mtukufu kuwafufua viumbe kutoka makaburini mwao, wataapa washirikina kwamba hawakukaa duniani isipokuwa kipindi kifupi. Watasema urongo katika kiapo chao kama walivyokuwa wakisema urongo duniani na wakiikataa haki ambayo Mitume walikuja nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net