Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 47

Ar-Room 30:47

الروم

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَآءُوهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَٱنتَقَمْنَا مِنَ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ ۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Na hakika tulikwishawatuma Mitume kabla yako kwa kaumu zao, na wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu wale waliofanya uhalifu. Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tulikwisha watuma Mitume kwa kaumu zao, na wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu wale walio fanya ukosefu. Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika tuliwatuma kabla yako wewe, ewe Mtume, Mitume waende kwa watu wao kwa kubashiria na kuonya, wawaite kwenye upwekeshaji (wa Allah Mtukufu) na wawatahadharishe na ushirikina. Wakawajia na miujiza na hoja zenye mwangaza, na wengi wao wakamkanusha Mola wao, na kwa hivyo tukawatesa wale waliotenda mabaya miongoni mwao, tukawaangamiza na tukawapa ushindi wafuasi wa Mitume. Na hivyo ndivyo tunavyowafanya wenye kukukanusha wanapoendelea kukukanusha na wasiamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net