Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 30 · Aya ya 28

Ar-Room 30:28

الروم

ضَرَبَ لَكُم مَّثَلًا مِّنْ أَنفُسِكُمْ ۖ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُم مِّن شُرَكَآءَ فِى مَا رَزَقْنَـٰكُمْ فَأَنتُمْ فِيهِ سَوَآءٌ تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنفُسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Maana

Amewapigia mfano kutokana na nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyoogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivyo tunazipambanua Aya zetu kwa watu watumiao akili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Amekupigieni mfano kutokana na nafsi zenu. Je! Katika hao iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyo kuruzukuni, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyo ogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivi tunazipambanua Aya zetu kwa watu wenye akili.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Amewapigia mfano, enyi washirikina, utokao na nafsi zenu: Je kuna yoyote, kati ya watumwa wenu na wajakazi wenu, anayeshirikiana na nyinyi katika riziki yenu na mkaona kuwa nyinyi na wao mko sawa katika hiyo, ikawa mnawaogopa wao kama mnavyowaogopa waungwana washirika katika ugawaji wa mali zenu? Nyinyi hamtaridhika na hilo, basi vipi mtaridhika na hilo upande wa Allah Mtukufu kwa kumfanya kuwa Ana mshirika miongoni mwa viumbe Vyake? Kwa mfano wa ufafanuzi huu, tunawafafanulia ushahidi na hoja watu wenye akili timamu ambao watanufaika nao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Room

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net