Ar-Room 30:21
الروموَمِنْ ءَايَـٰتِهِۦٓ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَٰجًا لِّتَسْكُنُوٓا۟ إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
Na katika Ishara zake ni kuwa aliwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye ameweka mapenzi na rehema baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaotafakari.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa alama zenye kuonyesha ukubwa Wake na ukamilifu wa uwezo wake ni kuwa Amewaumba wake kwa ajili yenu kutokana na jinsi yenu, enyi wanaume, ili nafsi zenu zijitulize kwao na ziburudike, na Akatia mapenzi na huruma baina ya mwanamke na mumewe. Hakika katika uumbaji huo wa Allah Mtukufu pana alama zenye kuonyesha uwezo wa Allah Mtukufu na kupwekeka Kwake kwa watu wenye kufikiria na kuzingatia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net