Aal-i-Imraan 3:86
آل عمرانكَيْفَ يَهْدِى ٱللَّهُ قَوْمًا كَفَرُوا۟ بَعْدَ إِيمَـٰنِهِمْ وَشَهِدُوٓا۟ أَنَّ ٱلرَّسُولَ حَقٌّ وَجَآءَهُمُ ٱلْبَيِّنَـٰتُ ۚ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Vipi Mwenyezi Mungu atawaongoa kaumu waliokufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawajia hoja zilizo wazi? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu ya madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu atawaongoaje watu walio kufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawafikia hoja zilizo wazi? Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. [86]
[86] Mwenyezi Mungu hakubaliani na watu walio kwisha shuhudia kuwa Mtume ni wa haki, na zikawajia dalili za kuonyesha hayo, kisha baada ya yote hayo wakamkataa, na wakakataa miujiza yake. Huo basi ni udhaalimu wao, na Mwenyezi Mungu hakubaliani na madhaalimu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Vipi Allah Mtukufu Atawaafikia wamuamini Yeye na wamfuate watu walioukanusha unabii wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, baada ya kuamini na kushuhudia kuwa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ni mkweli na yale aliyokuja nayo ni ya kweli na zikawajia wao hoja zinazotoka kwa Allah Mtukufu na dalili za usahihi wake? Na Allah Mtukufu Hawaafikii kwenye haki na usawa watu madhalimu, nao ni wale waliopotoka kwenye haki wakafuata batili, wakachagua ukafiri badala ya Imani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net