Al-Ankaboot 29:61
العنكبوتوَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
Na ukiwauliza; ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akafanya jua na mwezi kutiii amri yake? Bila ya shaka, watasema: Mwenyezi Mungu. Wapi basi wanakogeuzwa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ukiwauliza; Nani aliye umba mbingu na ardhi na akafanya jua na mwezi kuti'ii amri yake? Bila ya shaka, watasema: Mwenyezi Mungu. Wapi basi wanako geuzwa?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ukiwauliza, ewe Mtume, hao washirikina, Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi kwa mpango huu mzuri na akalidhalilisha jua na mwezi? Watasema, «Aliyeviumba hivyo ni Allah Mtukufu Peke Yake.» Basi vipi wao watapotoshwa waache kumuamini Allah Mtukufu, Muumba na Muendeshaji wa kila kitu, na wakawa wanamuabudu asiyekuwa Yeye? Basi uonee ajabu uzushi wao na urongo wao!
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net