Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 55

Al-Ankaboot 29:55

العنكبوت

يَوْمَ يَغْشَىٰهُمُ ٱلْعَذَابُ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِمْ وَيَقُولُ ذُوقُوا۟ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Siku itakapowafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao, na atasema, "Onjeni hayo mliyokuwa mkiyatenda!"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku itapo wafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao, na atasema: Onjeni hayo mliyo kuwa mkiyatenda!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hiyo Siku ya Kiyama, adhabu ya Jahanamu itawafunika makafiri upande wa juu wa vichwa vyao na upande wa chini wa nyayo zao. Hivyo basi Moto utawazunguka pande zao zote, na Allah Mtukufu Atasema kuwaambia wakati huo, «Onjeni malipo ya yale mliokuwa mkiyafanya ulimwenguni, ya kumshirikisha Allah Mtukufu na kufanya uhalifu na madhambi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net