Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 50

Al-Ankaboot 29:50

العنكبوت

وَقَالُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ ءَايَـٰتٌ مِّن رَّبِّهِۦ ۖ قُلْ إِنَّمَا ٱلْـَٔايَـٰتُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٌ مُّبِينٌ

Maana

Na walisema, "Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Sema, "Hakika Ishara ziko tu kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walisema: Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Ishara ziko kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na washirikina walisema, «Si ateremshiwe Muhammad dalili na hoja kutoka kwa Mola wake, kama vile ngamia wa Ṣãleḥ na fimbo ya Mûsã!» Waambie, «Jambo la miujiza hii liko kwa Allah Mtukufu, Akitaka Ataiteremsha na Akitaka Ataizuia. Na hakika ni kwamba mimi ni muonyaji, ninawatahadharisha na ukali wa adhabu Yake na mateso Yake, na ni mwenye kuwaonyesha njia ya haki na batili».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net