Al-Ankaboot 29:38
العنكبوتوَعَادًا وَثَمُودَا۟ وَقَد تَّبَيَّنَ لَكُم مِّن مَّسَـٰكِنِهِمْ ۖ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَعْمَـٰلَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَكَانُوا۟ مُسْتَبْصِرِينَ
Na pia kina A'di na Thamud. Nanyi yamekwisha wabainikia kutokana na maskani zao. Na Shetani aliwapambia vitendo vyao, na akawazuilia Njia, na hali walikuwa wenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pia kina A'di na Thamud. Nanyi yamekwisha kubainikieni kutokana na maskani zao. Na Shet'ani aliwapambia vitendo vyao, na akawazuilia Njia, na hali walikuwa wenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukawaangamiza kina ‘Ãd na Thamūd, na yameshaonekana na nyinyi magofu ya nyumba zao, vile yalivyokuwa matupu, hayana mtu yoyote katika wakazi wake, na vile mateso yetu yalivyowashukia wao wote. Na Shetani aliwapambia wao matendo yao maovu, na kwa hivyo akawazuia wasiifuate njia ya Allah Mtukufu na njia ya kumuamini Yeye na Mitume Wake, na walikuwa wakijiongoza kuona njia katika ukafiri wao na upotevu wao wakijifurahisha nayo, wakidhani kwamba wao wako kwenye uongofu na usawa, ilhali wao wamezama kwenye upotevu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net