Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 36

Al-Ankaboot 29:36

العنكبوت

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا فَقَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱرْجُوا۟ ٱلْيَوْمَ ٱلْـَٔاخِرَ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ

Maana

Na kwa Madyana tulimtuma ndugu yao Shuaibu, naye akasema, "Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu na iogopeni Siku ya Akhera, wala msiende katika ardhi mkifanya uharibifu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa Madyana tulimtuma ndugu yao Shuaibu, naye akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu na iogopeni Siku ya Akhera, wala msende katika ardhi mkifisidi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tulimtuma, kwa watu wa Madyan, ndugu yao, Shu‛ayb. Akawaambia, «Enyi watu wangu! Muabuduni Allah Mtukufu Peke Yake, na mumtakasie Ibada, kwani nyinyi hamna Mola isipokuwa Yeye. Na kuweni na matarajio mema, kwa ibada mnazofanya, kupata malipo mazuri ya Siku ya Akhera, na msifanye uharibifu na maasia kwa wingi, na msijikite juu ya hayo. Lakini tubieni kwa Allah Mtukufu kwa makosa hayo na mrudi Kwake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net