Al-Ankaboot 29:24
العنكبوتفَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوا۟ ٱقْتُلُوهُ أَوْ حَرِّقُوهُ فَأَنجَىٰهُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلنَّارِ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Basi haikuwa jawabu ya watu wake isipokuwa walisema, "Muueni au mchomeni moto!" Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwokoa kutokana na moto huo. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanaoamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila ni kusema: Muuweni au mchomeni moto! Mwenyezi Mungu akamwokoa na moto. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi jawabu la watu wa Ibrãhîm halikua isipokuwa ni kuambiana wao kwa wao, «Muueni au mchomeni kwa moto!» Wakamtupa motoni, na Allah Mtukufu Akamuokoa nao, na akaufanya kuwa ni baridi na salama kwake. Hakika katika kumuokoa kwetu Ibrãhîm kutokana na moto pana dalili na hoja kwa watu wanaomuamini Allah Mtukufu na kufanya matendo yanayoambatana na Sheria Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net