Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 12

Al-Ankaboot 29:12

العنكبوت

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّبِعُوا۟ سَبِيلَنَا وَلْنَحْمِلْ خَطَـٰيَـٰكُمْ وَمَا هُم بِحَـٰمِلِينَ مِنْ خَطَـٰيَـٰهُم مِّن شَىْءٍ ۖ إِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ

Maana

Na wale waliokufuru waliwaambia wale walioamini, "Fuateni njia yetu, nasi tutayabeba makosa yenu." Wala wao hawatabeba katika makosa yao chochote kile. Hakika hao ni waongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walio kufuru waliwaambia walio amini: Fuateni njia yetu, nasi tutayabeba makosa yenu. Wala wao hawatabeba katika makosa yao chochote kile. Hakika hao ni waongo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wamesema wale waliokataa upweke wa Allah Mtukufu miongoni mwa Makureshi, na wasiliamini onyo la Allah Mtukufu na ahadi Yake, kuwaambia wale waliomuamini Allah Mtukufu miongoni mwao na wakafuata Sharia Zake kivitendo, «Iacheni Dini ya Muhammad, na fuateni dini yetu, kwani sisi tutayabeba makosa yenu,» na wao si wenye kubeba chochote katika dhambi zao. Kwa kweli, wao ni warongo kwa yale waliyoyanena.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net