Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 10

Al-Ankaboot 29:10

العنكبوت

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ فَإِذَآ أُوذِىَ فِى ٱللَّهِ جَعَلَ فِتْنَةَ ٱلنَّاسِ كَعَذَابِ ٱللَّهِ وَلَئِن جَآءَ نَصْرٌ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمْ ۚ أَوَلَيْسَ ٱللَّهُ بِأَعْلَمَ بِمَا فِى صُدُورِ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Na katika watu yupo yule anayesema, "Tumemuamini Mwenyezi Mungu." Lakini anapopewa maudhi kwa sababu ya Mwenyezi Mungu, anayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapokuja nusura kutoka kwa Mola wako Mlezi, kwa yakini husema, "Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi." Kwani Mwenyezi Mungu hayajui zaidi yaliyomo vifuani mwa walimwengu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na katika watu wapo wanao sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu. Lakini wanapo pewa maudhi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wanayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapo kuja nusura kutoka kwa Mola wako Mlezi husema: Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi. Kwani Mwenyezi Mungu hayajui yaliomo vifuani mwa walimwengu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa watu, kuna wanaosema, «Tumemuamini Allah Mtukufu.» Na wafanyiwapo udhia na washirikina huwa wanapapatika kutokana na mateso yao na kero zao, kama wanavyopapatika kutokana na adhabu ya Allah Mtukufu na wasivumilie adhabu na mateso yake, wakaritadi na wakaiacha Imani yao. Na lau waja ushindi kutoka kwa Mola wako, ewe Mtume, kwa watu wenye kumuamini, watasema hawa wenye kuritadi kuiacha Imani yao, «Sisi tulikuwa pamoja na nyinyi, enyi Waumini, tukiwasaidia dhidi ya maadui wenu.» Je, si Allah Mtukufu ni Mjuzi zaidi kuliko yoyote wa kuyajua yaliyomo ndani ya vifua vya viumbe wake wote?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net