Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 53

Al-Qasas 28:53

القصص

وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِهِۦٓ إِنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّنَآ إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِۦ مُسْلِمِينَ

Maana

Na wanaposomewa, wanasema, "Tunaiamini. Hakika hii ndiyo Haki inayotoka kwa Mola wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu, tulionyenyekea."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo somewa wanasema: Tunaiamini. Hakika hii ni Haki inayo toka kwa Mola wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu, tulio nyenyekea. [53]

[53] Na hao wakisomewa Qur'ani hufanya haraka kutangaza Imani yao, na husema: Tumeyaamini hayo, kwani hayo ni Haki inayo toka kwa Mola wetu Mlezi; na sisi tulimjua Muhammad na Kitabu chake hata kabla ya kuteremka kwake, nasi tukanyenyekea kabla ya kusomwa kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi isomwapo hii Qur’ani kwa wale tuliowapa Kitabu wanasema, «Tumeiamini na tumeifuata kivitendo, hiyo ni haki itokayo kwa Mola wetu, hakika sisi tulikuwa, kabla haijateremka, ni Waislamu wenye kumpwekesha, kwani Dini ya Allah Mtukufu ni moja, nayo ni Uislamu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net