Al-Qasas 28:27
القصصقَالَ إِنِّىٓ أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ٱبْنَتَىَّ هَـٰتَيْنِ عَلَىٰٓ أَن تَأْجُرَنِى ثَمَـٰنِىَ حِجَجٍ ۖ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ ۖ وَمَآ أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ ۚ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Akasema, "Hakika mimi ninataka kukuoza mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa sharti kwamba unitumikie miaka minane. Lakini ukitimiza kumi, basi hiari ni yako. Nami sitaki kukutaabisha. Mwenyezi Mungu akipenda (Inshallah), utanikuta miongoni mwa watu wema."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Mimi nataka kukuoza mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane. Ukitimiza kumi, khiari yako; lakini mimi sitaki kukutaabisha. Inshallah utanikuta miongoni mwa watu wema. [27]
[27] Shuaibu a.s. akamwambia: Mimi nataka kukuoza mmoja wa hawa mabinti zangu kwa mahari ya kunifanyia kazi muda wa miaka minane. Ukitimiza kumi itakuwa ni khiari yako. Wala mimi sitaki kukulazimisha huo muda mrefu. Na Inshallah, Mwenyezi Mungu akipenda, utaniona mimi ni katika watu wema, wenye kwenda nawe kwa ihsani na kutimiza ahadi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mzee akasema kumwambia Mûsã, Mimi nataka kukuoza mmoja wa mabinti wangu hawa wawili, kwa sharti uwe muajiriwa wangu wa kuwachunga wanyama wangu kwa kipindi cha miaka minane. Na ukikamilisha miaka kumi, basi hiyo ni hisani yako. Na mimi sitaki kukusumbua kwa kuifanya miaka kumi. Utanikuta mimi, Allah Mtukufu Akitaka, ni miongoni mwa watu wema, katika uzuri wa tangamano na utekelezaji ahadi wa ninayoyasema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net