Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 20

Al-Qasas 28:20

القصص

وَجَآءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَا ٱلْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَـٰمُوسَىٰٓ إِنَّ ٱلْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَٱخْرُجْ إِنِّى لَكَ مِنَ ٱلنَّـٰصِحِينَ

Maana

Na akaja mbio mwanamume mmoja kutoka sehemu ya mbali mno ya mji, akasema, "Ewe Musa! Hakika, wakubwa wanashauriana juu yako kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa wanashauriana kukuuwa. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanao kupa nasaha. [20]

[20] Akaja mtu mmoja Muumini katika kaumu ya Firauni kutoka mwisho wa mji, ilipo enea khabari ya Musa kumuuwa Mmisri. Yule mtu akamwambia Musa kwamba watu wanapanga kutaka kumuuwa. Akamwambia: Toka mji, ukimbie usije ukauliwa! Hakika mimi ni katika wanao kupa nasaha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na akaja mtu mbiombio kutoka mwisho wa mji, akasema, «Ewe Mûsã! Kwa hakika wale wakubwa wa jamii ya Firáwn wanafanya njama ya kukuua na wanashauriana juu ya hilo, basi toka. Kwani mimi ni kati ya wale wanaokupa ushauri mzuri na wanaokupendelea wema».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net