Al-Qasas 28:18
القصصفَأَصْبَحَ فِى ٱلْمَدِينَةِ خَآئِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا ٱلَّذِى ٱسْتَنصَرَهُۥ بِٱلْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُۥ ۚ قَالَ لَهُۥ مُوسَىٰٓ إِنَّكَ لَغَوِىٌّ مُّبِينٌ
Akapambazukiwa mjini asubuhi naye ana hofu, akiangalia huku na huku. Mara yule yule aliyemtaka msaada jana akawa anamuita kwa sauti kubwa amsaidie. Musa akamwambia, "Hakika wewe ni mgomvi kweli kweli."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akapambazukiwa mjini asubuhi naye ana khofu, akiangalia huku na huku. Mara yule yule aliye mtaka msaada jana akawa anampigia kelele amsaidie. Musa akamwambia: Hakika wewe ni mgomvi kweli kweli. [18]
[18] Kulipo pambazuka asubuhi Musa alikuwapo mjini, Misri, naye yumo katika khofu, akitaraji kufikiwa na madhara kutokana na watu kwa sababu vile alivyo muuwa Mmisri. Akamwona yule Muisraili aliye mtaka msaada jana, naye akamtaka msaada mara ya pili katika ugomvi na Mmisri mwengine. Musa akamkemea kwa kumwambia: Hakika wewe mtu matata mno, na dhaahiri wewe ni mpotovu. Unafanya yale yale uliyo yafanya jana, na unaniita tena nikusaidie!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hivyo basi Mûsã akaingiwa na hofu akiwa kwenye mji wa Firáwn, anatafuta habari zinazozungumzwa na watu kuhusu yeye na yule mtu aliyemuua, hapo akamuona yule mtu wake wa jana akipigana na Mmisri mwingine na akimtaka amsaidie. Mûsã alimwambia, «Kwa kweli, wewe ni mwingi wa upotofu, ni mpotevu wa waziwazi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net