Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 27 · Aya ya 85

An-Naml 27:85

النمل

وَوَقَعَ ٱلْقَوْلُ عَلَيْهِم بِمَا ظَلَمُوا۟ فَهُمْ لَا يَنطِقُونَ

Maana

Na kauli itawaangukia juu yao kwa vile walivyodhulumu. Basi hao hawatatamka lolote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kauli itawaangukia juu yao kwa vile walivyo dhulumu. Basi hao hawatasema lolote. [85]

[85] Na adhabu itawateremkia kwa sababu ya kujidhulumu nafsi zao kwa ukafiri. Basi watakuwa hawawezi kujilinda wala kutaka udhuru.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo lithibiti juu yao neno la adhabu kwa sababu ya udhalimu wao na ukanushaji wao, na watakuwa hawatamki neno lenye hoja ya wao kujitetea nafsi zao ili kujiepushia adhabu kali iliyowashukia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Naml

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net